Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:45

Obama amunga mkono Hillary Clinton


Obama DEM 2016 Clinton
Obama DEM 2016 Clinton

Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza rasmi kwamba anamunga mkono Hillary Clinton kama mgombea wa kiti cha rais kwa niaba ya chama cha Democratic, na kutoa wito kwa Wademocrats kuungana pamoja kuchagua rais.

Katika ujumbe wa video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook, wa Bi Clinton, Obama anasema "sidhani kumewahi kuwepo na mtu aliyena ujuzi kama yeye kuongoza ofisi hii."

Rais Obama anasema anasubiri tu kuanza kua na jukumu muhimu katika mashindano ya atakae chukua nafasi yake na utawala wame umekua na mazungumzo na washauri wa Bi. Clinton hivi karibuni juu ya jinsi na namna atakavyoweza kumsaidia.

Tangazo hilo limetolewa muda mfupi baada ya Rais Obama kukutana na Bernie Sanders aliyeshindwa na Clinton lakini amesema hatositisha kampeni yake hadi mkutano mkuu wa Julai.

Rais Obama amempongeza Sanders na Clinton kwa kampeni kabambe walofanya na kusema wameinua hadhi ya chama chao na kuwataka kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha ushindi wa chama cha.

XS
SM
MD
LG