Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:20

Clinton afikisha wajumbe wanaohitajika kuwa mgombea urais


Bi.Hillary Clinton akihutubia wafuasi wake.
Bi.Hillary Clinton akihutubia wafuasi wake.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Bi Hillary Clinton anaweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa mtarajiwa wa ugombea rais wa moja ya vyama vikubwa vya siasa Marekani.

Hato-tatangazwa rasmi kuwa mgombea wa chama cha Demokrat mpaka katika mkutano mkuu mwezi ujao, lakini mpaka sasa ameshafikisha idadi ya wajumbe 2,383 wanaohitajika kuteuliwa kuwa mwakilishi wa chama na kumshinda Seneta wa Vermont Bernie Sanders.

John Hudak, naibu mkurugenzi wa kituo cha ufanisi wa uongozi wa umma katika taasisi ya Brookings ameiambia VOA kwamba umuhimu wa tukio hilo unaweza usipewe uzito unaohitajika kwa kuwa Bi.Clinton toka mwanzo anafahamika na aliingia katika kinyang'anyiro akitarajiwa atakuwa mshindi.

Bi. Clinton alipopata habari hizo Jumatatu usiku alitahadharisha wafuasi wake akisema ingawa hesabu za vyombo vya habari zinampatia idadi ya wagombea wanaohitajika ikiwa ni tukio ambalo halijawahi kutokea lakini kungali kuna mashindano katika majimbo sita yaliyobaki kufanyika siku ya Jumanne na kwamba anapigana kwa nguvu kupata kila kura katika mashindano hayo.

Jumanne ni siku ya mwisho ya utaratibu wa uchaguzi wa awali ambapo kuna wajumbe 851 waliobaki kupiganiwa upande wa chama cha Democratic.

XS
SM
MD
LG