Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa amri ya kukamatwa kwa mmiliki wai jengo la gorofa saba lililoanguka huko Nairobi na kusababisha vifo vya watu 14 na wengine wengi kujeruhiwa.
Rais Kenyatta aliyetembelea eneo la ajali ametaka uchunguzi ufanyika katika majengo ya karibu ili kuthibitisha ziko katika hali ya usalama.
Waokozi katika mji mkuu wa Kenya wanaendelea kuwatafuta watu ambao huwenda wamenasa ndani ya vifusi vya jengo hilo lililoanguka kutokana na mafuriko.
Maafisa wa BNairobi wanasema zaidi ya watu 120 waliokolewa na kupelekwa hospitali baada ya kujeruhiwa. Chama cha Msalaba Mwekundu kinaeleza kwamba watu katika nyumba na majengo jirani yameathiriwa kutokana na kuanguka jengo hilo Ijuma usiku.