Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:53

Marubani wa Kenya Airways warudi kazini


Ndege ya Kenya Airways
Ndege ya Kenya Airways

Marubani wa shirika la ndege la Kenya Airways wanatarajiwa kurudi kazini siku ya Ijuma baada ya kufikia makubaliano na wakuu wa shirika hilo juu ya madai yao ya kufukuzwa mkuu wa shirika lao.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kenya Airways Bi.Wanjiku Mugo, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba ingawa hawezi kuthibitisha tunapozungumaza, lakini wamepata habari kweamba marubani watarudi kazini kuanzia Ijuma asubuhi, lakini wanasubiri kupatqa taarifa rasmi kutoka chama chao cha marubani Kenya KALPA.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:32 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Marubani wanadai kufukuzwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Airways Mbuvi Ngunze kutokana na mpango wake wa kufanya marekebisho ili kuokoa shirika hilo linalokumbwa na matatizo ya kifedha.

Katibu Mkuu wa KALPA Paul Gichinga ameiambia Sauti ya Amerika kwamba hawawezi kueleza makubaliano yaliyofikiwa bado lakini wameridhika kutokana na kwamba wakuu wa shirika hilo wamekubaliana na baadhi ya madai yao.

XS
SM
MD
LG