Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 00:01

Wabunge wa Brazil waunga mkono rais kufungliwa mashtaka


Wabunge wa Baraza Kuu wanaounga mkono kufunguliwa mashtaka rais wakikusanyika pamoja wakati bwa mjadala wa bunge. mjini Brasilia, Brazil, April 15, 2016.

Wafuasi wa upinzani huko Brazil walisherehekea usiku mzima Jumapili baada ya wabunge kufanikiwa kuidhinisha hoja ya kuanzishwa utaratibu wa kumfungulia mashtaka Rais Dilma Rousseff.

Saa chache baada ya Rais Rouisseff kupata pigo hilo, mwanasheria mkuu Jose Eduardo Cardozo, anaeongoza tume ya mawakili wake, anasema kiongozi huyo anaekabiliwa na matatizo yuko tayari kwa majadiliano :"chini ya misingi ya kidemokrasia".

Wapinzani wa serikali wakisubiri nje ya bunge wakati wabunge wapiga kura
Wapinzani wa serikali wakisubiri nje ya bunge wakati wabunge wapiga kura

Watetezi wa Bi. Rousseff wamedai kwamba juhudi za kumfungulia mashtaka ni sawa na jaribio la mapinduzi lililopangwa na maadui wake wa kisiasa.

Ukumbi wa Baraza Kuu la bunge lilishuhudia makelele kuzomeana na furaha wakati wabunge walipokua wanapiga kura ya wazi kupitisha hoja hiyo huku bendera ya Brazil ikipeperushwa na wabunge wote wa upinzani ndani ya ukumbini huo baada ya kura 342 kupatikana, kufuatia siku tatu za mjadala juu ya hoja hiyo.

Hatimae ni wabunge 367 walounga mkono kufunguliwa mashtaka dhidi ya wabunge 137 walopinga, na wabunge 7 hawakushiriki.

Wafuasi wa serikali wakitizama wabunge wakipiga kura.
Wafuasi wa serikali wakitizama wabunge wakipiga kura.

Hoja hiyo hivi sasa inapelekwa mbele ya Baraza la senet. Ikiwa baraza hilo litapitisha hoja kwa wingi mdogo tu hapo mapema mwezi May, basi Bi. Rousseff atasitishwa kazi kwa siku 180 na nafasi yake kuchukuliwa na Makamu Rais Michel Temer, atakae kua kaimu rais hadi kesi yake kukamilika.

Temer atakamilisha muda wa mhula wa Rousseff unaomalizika 2018 ikiwa atapatikana na hatia.Hata hivyo wakili wake Cardozo anasema atawasilisha ushahidi mbele ya Senet jambo ambalo halifanyika katika baraza kuu.

XS
SM
MD
LG