Mchezaji mashuhuri wa mpira wa vikapu Marekani Kobe Bryant acheza mchezo wake wa mwisho, Jumatano usiku mjini Los Angeles, akifunga ukurasa wa kihistoria wa miaka 20 kucheza katika ligi ya NBA kwa kishindo.
Bryant mwenye umri wa miaka 37 alipachika pointi 60 ikiwa ni nyingi kabisa katika msimu huu kwake yeye na kuipatia timu yake ya Lakers ushindi wa 101 kwa 96 dhidi ya wageni wao Utha Jazz, mbele ya maelfu ya mashabiki kwenye uwanja wa Staples Center na mamilioni ya watazamaji na mashabiki kote duniani.
Bryant aliyejulikana pia kama "The Black Mamba" alichezea Lakers kwa miaka 20 na kua mchezaji aliyebaki katika timu moja kwa muda mrefu zaidi katika historia ya NBA.
na matukiko mengine ya kihistoria ni kunyakua taji mara tano ya timu bingwa, mara tatu ikiwa ni mfululizo kati ya 2000 - 2001, akitajwa mchezaji bora wa michuano ya finali mara mbili mfululizo.
Anakua mchezaji wa tatu wa NBA kupachika pointi nyingi akiwa nafasi moja na bingwa Michael Johnson. Kwa ujumla amepachika pointi m33,643, ambapo katika michuano 25 amepata zaidi ya pointi 50, ikiwa ni pamoja na mc hezo wake wa mwisho wa Jumatano.
Warriors wavunja rikodi ya ushindi NBA
Ukurasa mwengine wa historia katika NBA uliandikwa Jumatano usiku pale timu ya Golden State Warriors kuvunja rikodi ya NBA ya ushindi mwingi kabisa mnamo msimu moja kwa kuilaza Memphis GFrizzlies 125 - 104 na kuimaliza msimu ikiwa na ushindi 73 na kushindwa mara 9 pekee.
Ushindi huo wa Jumatano umevunja rikodi iliyowekwa na timu ya Chicago Bulls ya mwaka 1995-96 iliyongozwa na Michael Jordan.
Nyota wa Warriors Stephen Curry alivunja pia rikodi nyingine binafsi na kua mchezaji wa kwanza katiika historia ya mpira wa vikapu kupachika pointi 400 kutokana na kutumbukiza wavuni mpira kutoka eneo la pointi tatu.