Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:37

Viongozi wa kiafrikia watajwa katika hati za Panama


Panama Papers
Panama Papers

Hati zinazoelezwa kua na takwimu nyingi zaidi za akaunti za matajiri kuwahi kutolewa kwa siri duniani, zinaonesha jinsi wanasiasa 143 wakiwemo viongozi 12, walivyotumia vituo vya kukwepa kodi nchje ya nchi zao na njia nyenginezo za kukwepo ushuru na vikwazo.

Baadhi ya viongozi na wanasiasa wa Afrika walotajwa katika hati hizo zilziotolewa kwa siri ni pamoja na binamu wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, dada pacha wa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, gavana wa zamani aliyekizuizini wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Delta huko Nigeria na waziri wa mafuta wa Angola.

Stanley Achonu wa kundi la kiraia linaloshughulikia kazi za kufanya mabadiliko kwenye bajeti ya taifa ya Nigeria, anasema utumiaji wa taasisi za kigeni katika mataifa ya visiwa si jambo la uhalifu, lakini kutolewa kwa hati hizo kunathibitisha kile waafrika wamekua wakijua wakati wote kwamba viongozi wao wamekua wakitumia akaunti hizo za nje kuficha fedha za umaa walizoibia.

Miongoni mwa waafrika wengine walotajwa ni naibu mwanasheria mkuu wa Kenya, Kalpana Rawal na mjane wa rais wazamani wa Guine Lansana Conte, Bi. Mamadie Toure.

XS
SM
MD
LG