Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:03

Wanachama wa CCM Zanzibar washerehekea ushindi wa Shein


Wafusai wa chama tawala cha CCN huko Zanzibar wakisherehekea ushindi wa Rais Ali Mohamed Shein Machi 21, 2016
Wafusai wa chama tawala cha CCN huko Zanzibar wakisherehekea ushindi wa Rais Ali Mohamed Shein Machi 21, 2016

Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC imemtangaza Dr Ali Mohamed Shein kua mshindi wa uchaguzi wa marudio wa rais ulofanyika jumapili na kususiwa na chama kikuu cha upinzani CUF.

Akitangaza matokeo hayo Jumatatu mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha amesema Rais Shein alipata kura 299, 982 ikiwa sawa na asili mia 91.4 za kura zote.

Kiongozi wa upinzani wa chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamadi alipata kura 6,076, na Bw. Jecha anasema majina ya wagombea wote wa uchaguzi wa oktoba 25 yalikua katika vyeti vya kupiga kura kutokana na kwamba hakuna mgombea aliyewasilisha rasmi hati za kusema hatoshiriki katika uchaguzi huo.

Wafuasi wa CCM wakisherehekea ushindi wa Dr. Shein
Wafuasi wa CCM wakisherehekea ushindi wa Dr. Shein

Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo wafuasi wa chama tawala cha CCM walishuka katika mitaa ya Ubguja na kusherehekea ushindi huo.

Nafasi ya pili katika uchaguzi huo ilichukuliwa na Hamad Rashid Mohamed wa chama cha ADC aliyepata asili mia 3 za kura. Mwandishi wa sauti ya Amerika huko Zanzibar anaripoti kwamba kutokana na ususiaji wa upinzani idadi kubwa ya wapiga kura hawakujitokeza Jumapili kushiriki katika zowezi la kupiga kura hasa katika kisiwa cha Pemba.

Cheti ya matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar 2016
Cheti ya matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar 2016

Serikali ya Zanzibar imetangaza kwamba hakutakua na serikali ya umoja wa kitaifa kama inavyoelezwa kwenye katiba mpya ya visiwa hivyo kutokana na kwamba hakuna chama cha kingine kilichopata zaidi ya asili mia 10 za kura kuweza kuunda serikali ya umoja.

XS
SM
MD
LG