Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 04:43

Wacuba wajitayarisha kumpokea Obama


Magari ya zamani ya Marekani yanatumiwa kusafirisha watali mjini Havana, Cuba, March 18, 2016.
Magari ya zamani ya Marekani yanatumiwa kusafirisha watali mjini Havana, Cuba, March 18, 2016.

Serikali ya Cuba na wananchi wanamsubiri kwa hamu Rais Barack Obama akianza ziara yake ya kihistoria kisiwani humo siku ya Jumapili, akiwa rais wa kwanza wa Marekani kulitembelea taifa hilo jirani katika kipindi cha miaka 90 iliyopita.

Wananchi wamegawika kutokana na ziara hiyo, baadhi wakiwa na matumiani kwamba ni tukio la kihstoria kupelekea kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi vya Marekani, na kuna wale wanaoamini hakuna kitakacho badilika chini ya utawala wa kikomunisti.

Baiskeli inayotumiwa kama teksi imepambwa bendera za Marekani na Cuba
Baiskeli inayotumiwa kama teksi imepambwa bendera za Marekani na Cuba

Matarajio

Kuna Wacuba kama Yosleny Borroto, anaechukulia ziara hiyo ya kwanza na kiongozi wa Marekani tangu miana ya 1920 ni ishara ya mabadiliko makubwa katika nchi yake.

"Amekua moja wapo ya marais wa Marekani wanaotaka kutusaidia.. kutusiadia ili nchi yetu ipate maendeleo." alisema Borroto.

Rais Obama anafuatana na baadhi ya wafanyabiashara ikiwa ni ishara ya kuzungumzia masuala ya mikataba mipya ya biashara ingawa vikwazo vya kiuchumi vitaendelea kutekelezwa hadi bunge la Marekani kukubali kuviondowa

Watali wakitembea katika mtaa wa Vedado mjini Havana, Cuba
Watali wakitembea katika mtaa wa Vedado mjini Havana, Cuba

Wasi wasi hakuna kitakacho badilika

Lakini wakati huo huo kuna Wacuba wenye wasi wasi kama Oscar Casanella Saint Blancard, anaehisi analengwa na serikali kutokana na urafiki wake na wapinzani. Ana hofu kwamba kuanzishwa kwa uhusiano kamili wa kidiplomasia kati ya Washington na Havana hautamanisha mabadiliko makubwa bali yake anadhani kutakua na matatizo zaidi.

"Suala la kwanza, serikali ya Cuba itakua na tabia gani baada wa ziara, haitotosha kuondowa vikwazo hivyo vya marekani. Kwa sababu kuna vikwazo vya serikali ya Cuba dhidi ya watu wa Cuba, na ninadhani hivyo ndivyo hatari zaidi ." alisema Casanella.

Mwanaharakati wa haki za binadam Cuba Miriam Leiva mjini Havana
Mwanaharakati wa haki za binadam Cuba Miriam Leiva mjini Havana

Wapinzani

Nao wapinzani wakuu wa serikali wamefurahishwa na juhudi za rais Obama. Mpizani Miriam Leiva anasema akiweza kukutana na rais Obama basi atamuambia "nina kushukuru kwa sera zako kuelekea kisiwa chetu ambazo zitaleta afuweni kwa maisha ya Wacuba".

Maafisa wa white House wanasema miongoni mwa vipaumbele vya ziara yake ni kukutaka na wanaharakati wanaotetea demokrasia huko Cuba.

XS
SM
MD
LG