Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:51

Marekani inailaumu Syria kujaribu kuvuruga mazungumzo


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry akikutana na wenzake wa Ufraansa, Uingereza, Ujerumani na Utaliana mjini Paris., Ufaransa, March, 13, 2016.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry akikutana na wenzake wa Ufraansa, Uingereza, Ujerumani na Utaliana mjini Paris., Ufaransa, March, 13, 2016.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry ameilaumu Syria siku ya Jumapili, kwa "kujaribu kuvuruga kwa maksudi" mazungumzo ya amani yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa, yenye lengo la kumaliza miaka mitano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Anasema pendekezo la serikai ya Damuscus la kutokuwepo na mazungumzo juu ya kuondolewa madarakani Rais Bashar al-Assad ni jambo lililoweza kuharibu mazungumzo hayo.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani amesema kwamba, ghasia katika nchi hiyo iliyoharibiwa kwa vita zimepunguka sana, kufikia asili mia 80 hadi 90, tangu kutekelezwa makubaliano ya kusitisha mapigano wiki mbili zilizopita.

Lakini Bw. Kerry anasema mkiukaji mkuu wa makubaliano hayo ni utawala wa Assad, anasema "ni lazima mashambulizi ya mabomu kutoka angani yasitishwe."

Kerry alizungumza baada ya kukutana na wenzake wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Utaliana siku ya Jumapili mjini Paris juu ya mzozo huo wa Syria siku moja kabla ya kuanza mazunguzmo ya amani ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

XS
SM
MD
LG