Maelfu ya waombolezi wahudhuria mazishi ya mwanasiasa mashuhuri wa Sudan, Hassan al-Turabi, aliyezikwa Jumapili Machi 6, 2016, katika makaburi mashariki ya mji mkuu wa Khartoum.
Kiongozi huyo wa kislamu na mpinzani mkuu wa serikali, alifariki Jumamosi kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 84. Maafisa wakuu wa serikali walihudhuria pia mazishi hayo.
Turabi alikua na jukumu kubwa katika mapinduzi ya 1989 yaliyomweka madarakani Rais Omar al-Bashir.
Hata hivyo, marafiki hao wawili walikuja kugombana na kua mahasimu, na Turabi alikua mwanasiasa pekee wa Sudan kuunga mkono hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa kiongozi huyo kwa tuhuma za uhalifu wa vita.
Aliwekwa jela mara kadhaa baada ya ugomvi wa kupigania madaraka na kugombana na Bashir 1999.