Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 17, 2025 Local time: 08:13

Ndulu: Barclays haiondoki Tanzania


Wateja wasubiri nje ya tawi la benki ya Barclays Bank kufunguliwa mjini London, Feb. 12, 2013.
Wateja wasubiri nje ya tawi la benki ya Barclays Bank kufunguliwa mjini London, Feb. 12, 2013.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Benno Ndulu, anasema benki mashuhuri ya Uingereza Barclays haiondoki Tanzania licha ya kwamba ilitangaza Jumanne kwamba inauza zaidi ya asili mia 62 ya biashara zake barani Afrika.

Profesa Ndulu anasema Barclays imeamua kupunguza hisa zake barani humo kwa sababu ya kukabiliana na hasara walokua wanapata katika mazingira ya hatari katika baadhi ya biashara zao ili kuweza kuimarisha faida na usimamizi wa benki hiyo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:02 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

"Suala la kupunguza huduma", anasema Ndulu," sio upande wa Barclays pekee, kwa ujumla benki kubwa nyingi zimekua zikipata adhabu kutoka kwa wasimamizi wao kwa ajili ya kufanya biashara katika mazingira ambayo wao wanaona ni ya hatari"

Kutokana na hali hiyo benki za dunia zinapunguza huduma zake katika nchi ambazo zinatiliwa shaka kua ni ya hatari kufanya biashara. Lakini kwa upande wa Tanzania mkuu wa benki anasema wamearifiwa kwamba Barclays hawataondoka kwa wakati huu.

XS
SM
MD
LG