Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 18:31

Milipuko miwili yauwa watu 18 Baidoa, Somalia


Kati kati wa mji wa baidoa Somalia
Kati kati wa mji wa baidoa Somalia

Milipuko miwili mikubwa imeutikisa mji wa pwani wa Somalia wa Baidoa km 245 magharibi ya mji mkuu Mogadishu.

Maafisa wa afya wameiambia Sauti ya Amerika kwamba mili ya watu 18 imepatikana kutokana na milipuko hiyo na kuna watu wengi wanahofiwa walojeruhiwa.

Shambulizi la kwanza linaloaminika lilikua ni bomu lililotegwa ndani ya gari lilitokea karibu na soko kuu la mji huo, na shahidi mmoja ameiambia VOA kwamba mlipuko ulitokea karibu na hoteli ya Baidoa.

Na muda mchache baadae mlipuko mwengine ulofanywa na mjitoa mhanga ulitokea kwenye mgahawa kati kati ya mji.

Mlipuko huo unatokea wakati viongozi wa mataifa yanayochangia kikosi cha kulinda amani Somalia AMISOM wanakutana Djibouti kutamini mkakati wa kupambana na kundi la Al-Shabab.

XS
SM
MD
LG