Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 20:07

Watu 12 wameuwawa Somalia


Raia wa somalia wakitembea karibu na jengo lililoharibiwa na milipuko.
Raia wa somalia wakitembea karibu na jengo lililoharibiwa na milipuko.

Kundi la Al shabab limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Takriban watu 12 wameuwawa na wengine 30 wamejeruhiwa katika mashambulizi mawili makubwa ya mlipuko na risasi kwenye mji mkuu wa Somalia Ijumaa jioni.

Kundi la Al shabab limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Mashahidi wanaripoti kuwa gari kubwa lililokuwa limejaa milipuko lilitegua mabomu katika eneo la ukaguzi karibu na hoteli ya SYL huko Mogadishu.

Waziri wa usalama wa Somali Abdirizak Omar Mohamed ameiambia idhaa ya kisomali ya VOA kwamba wanachama watano wa shirika la taifa la usalama waliuwawa katika kituo cha ukaguzi wakati wa shambulizi hilo. Amesema mshambuliaji aliyekuwa anaendesha gari lenye milipuko pia alikufa.

Muda mfupi baadae, watu watatu waliokuwa na bunduki walitoka nje ya gari na kuanza kufyatua risasi katika jaribio la kulazimisha njia ya kuingia kwenye hoteli lakini vikosi vya usalama viliwazuiya.

Mohamed amesema walinzi na vikosi vya usalama katika hoteli waliwafyatulia srisasi na kuwauwa wanamgambo watatu kabla hawajaingia kwenye hoteli. Mashahidi wamethibitisha kwamba wanamgambo wa Al shabab hawakuweza kuingia ndani ya hoteli.

XS
SM
MD
LG