Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 20:22

Rajabu apongeza juhudi za kimataifa kutanzua mzozo wa Burundi


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, kulia, anamsikiliza Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi akizungumza wakati wa mkutano na waandishi habari mjini Bujumbura, Burundi, Feb. 23, 2016.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, kulia, anamsikiliza Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi akizungumza wakati wa mkutano na waandishi habari mjini Bujumbura, Burundi, Feb. 23, 2016.

Mwenyekiti wa zamani wa chama tawala cha Burundi CNDD-FDD, anaeishi uhamishoini Hussein Radjabu amepongeza juhudi zinazofanywa na viongozi mbali mbali katika kujaribu kupata suluhisho kwa mzozo wa kisiasa wa Burundi.

Hussein Radjabu azugumzia ziara ya Ban Bujumbura
please wait

No media source currently available

0:00 0:08:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizungumza baada ya ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon nchini Burundi siku ya Jumanne, Bw. Radjabu anasema, hakuna njia nyingine iliyobaki isipokua kufanyika mazungumzo kati ya pande zote zinazohusika.

Kiongozi huyo anaejaribu kuunganisha upinzani wa Burundi ili uwe na sauti moja anasema, Rais Pierre Nkurunziza alikubali kwa shingo upande kufanyika kwa mazungumzo lakini hadhani ana nia ya dhati kutanzua mzozo huo kati ya warundi, bila ya shinikizo la kimataifa.

Alipotembelea Burundi siku ya Jumanne Bw. Ban alikutana na wajumbe wa upinzani, viongozi wa asasi za kiraia pamoja na rais Nkurunziza na kuwapa wote ujumbe mmoja, kuwataka kuanza mazungumzo bila ya masharti yeyote.

XS
SM
MD
LG