Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 01:09

Museveni ashinda uchaguzi wa rais Uganda


Museveni Uganda Election
Museveni Uganda Election

Rais Yoweri Museveni amemeshinda uchaguzi wa rais ulokua na utata na ghasia, kufuatana na tangazo la tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, na hivyo kumrudisha madarakani baada ya kuliongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa zaidi ya miaka 30.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Badru Kiggundu alitangaza mchana wa hii leo "Tume inatangaza kwamba Yoweri Kaguta Museveni amechaguliwa kua rais wa Jamhuri ya Uganda."

Kufuatana na taarifa hiyo Museveni amepata asili mia 60.8 za kura akimshinda mpinzani wake mkuu Kizza Besigye aliyepata asili mia 35.4.

Wafuatiliaji wa Umoja wa Ulaya na Jumuia ya Madola wamekosoa jinsi uchaguzi ulivyofanyika na Besigye amepinga matokeo hayo. Mkuu wa wafuatliaji wa EU Eduard Kukan amesema "uchaguzi haukua wa huru, wazi, au wa kuaminika."

XS
SM
MD
LG