Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 04:31

Korea Kaskazini yalaaniwa na jumuia ya kimataifa kwa kufyetua roketi


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akitizama kufyetuliwa kwa roketi katika picha hiyo isiyojulikana imepigwa lini iliyotolkewa na shirika habari la (KCNA) mjini Pyongyang, Feb. 7, 2016.

Korea ya Kaskazini imefyetua roketi ya masafa ya mbali siku ya Jumapili ikibeba kile inachodai ni mtambo wa setaliti angani, ikikaidi vikwazo vya Umoja wa Mataifa vinavyoipiga marufuku kufyetua makombora ya masafa marefu.

Roketi ilifyetuliwa kutoka kituo cha kufyetua setaliti cha Tongchang-ri karibu na mpaka wake na China upande wa kaskazini magharibi. Serikali ya Korea ya Kaskazini ilitoa taarifa baadae kupitia shirika lake rasmi la habari KCNA kwamba ufyetuliaji umefanikiwa.

Taarifa imeeleza kwamba, "Wanasayansi na wahandisi wa taifa wamefanikiwa kusafirisha na kuweka angani setaliti iliyopewa jina la Gwangmyongson-4, chombo kilichotengenezwa chini ya mpango wa kitaifa wa miaka mitano wa 2016."

Roketi ya Korea Kaskazini ikipaa angani
Roketi ya Korea Kaskazini ikipaa angani

Serikali ya Pyongyang inadai kwamba kufyetuliwa roketi hiyo ni sehemu ya mpango wake wa amani wa angani ili kusafirisha mitambo yake ya setaliti kwenye anga za juu.

Hata hivyo mpango wa anga za juu wa taifa hilo umelaaniwa duniani kama ni uchochezi wa kuendeleza teknolojia yake ya nuklia na makombora ya masafa marefu.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amesema kufyetuliwa kwa roketi hiyo haihatarisi tu usalama wa raia wa Korea zote mbili bali pia ule wa kanda nzima pamoja na Marekani.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutaka kwa kikao cha dharura Jumapili kujadili kitendo hicho cha Korea Kaskazini kutokana na ombi kutoka Marekani, Japan na Korea ya Kusini.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-Moon anasema ni jambo la kulaaniwa kwamba Korea Kaskazini imefyetua roketi ikitumia teknolojia yake ya makombora ya masafa marefu ikikuka maazimio ya Baraza la Usalama.

XS
SM
MD
LG