Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:29

Kenya yathibitisha wanajeshi wake kuuwawa na Al shabab


Wanamgambo wa Al shabab
Wanamgambo wa Al shabab

Rais Kenyatta amesema nchi yake haitawaogopa Al Shabab na kuweka bayana kwamba Kenya itawashughulikia wahalifu hao waliohusika na shambulizi hilo nchini Somalia na damu ya wanajeshi hao haitopotea bure.

Rais wa Kenya, Uhuru Kunyatta amesema wanajeshi kadhaa wa Kenya wameuliwa baada ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la Somalia, Al-Shabab kushambulia kambi ya jeshi.

Imeelezwa kambi hinyo ni ya Umoja wa Afrika iliyopo katika mji wa El-Adde unaopatikana takriban kilometa 60 kusini mwa mji mkuu wa eneo la Garbaharey.

Rais Kenyatta amesema nchi yake haitawaogopa Al Shabab na kuweka bayana kwamba Kenya itawashughulikia wahalifu hao waliohusika na shambulizi hilo nchini Somalia na damu ya wanajeshi hao haitopotea bure.

Ameongeza kusema Kenya na washirika wake wataendelea kubaki nchini Somalia kukamilisha mpango utliowapeleka huko.

Wapiganaji wa Al Shabab walivamia lango kuu la kambi hiyo wakiwa na takriban magari manne yakiwa na milipuko na kufuatiwa kurushiana risasi baina ya washambuliaji na wanajeshi wa Kenya ambao walikuwepo kambini hapo.

Kwa mujibu wa kundi la Al-Shabab, linadai limewaua wanajeshi 60 wa vikosi vya Kenya.

Lakini Naibu Gavana wa Gedo, Mohamed Hussein Isaakameiambia VOA kwamba wanajeshi wa Kenya waliouliwa ni kati ya 35 na 40 na vikosi vingine vilifanikiwa kukimbia kutoka kambini hapo.

Isaak vilevile amesema ndege za kivita za Kenya zilirusha mambomu kwa wapiganaji wa Al Shabab kuzunguka mji wa El-Adde na kuharibu magari mawili yaliyokuwa na silaha.

Mashuhuda wanasema Al-Shabab walipandisha bendera yao baada ya kulitwaa eneo hilo na kushikilia silaha katika magari ya kivita.

Misheni ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia AMISOM imethibitisha tukio hilo japokuwa haikutoa taarifa za kina.

Katika taarifa yake, waziri wa usalama wa Somalia Abdiqadir Aheikh Ali Dinii ameshutumu shambulizi hilo katika kambi ya Umoja wa Afrika.

XS
SM
MD
LG