Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 18:19

Milipuko, Milio ya Bunduki yatikisa kati kati ya Jakatra


Maafisa wa polisi wa Indonesia waonekana wakikabiliana na mashambulizi ya bunduki mjini Jakatra januari 14, 2016
Maafisa wa polisi wa Indonesia waonekana wakikabiliana na mashambulizi ya bunduki mjini Jakatra januari 14, 2016

Wanamgambo wamelipua mabomu kwa mfululizo katika mji mkuu wa Indonesia, Jakatra Alhamisi asubuhi, kufuatana na maafisa wa usalama na mashahidi, na kufanya mfululizo wa mashambulizi ya bunduki na polisi na kusababisha vifo vya watu sita.

Ghasia zilianza asubuhi kati kati ya Jakatra, katika mtaa wenye jengo la maduka ya fahari, hoteli za kifahari, ofisi za ubalozi na majengo mengine. Kwa ujumla inaripotiwa kumekuwepo na milipuko sita.

Mashahidi wanasema baadhi ya milipuko ilifanywa na watu walojitoa mhanga kulipua mabomu, ingawa baadhi ya maafisa wa polisi wamekanusha jambo hilo wakisema badala yake, huwenda ilikua ni magruneti ndiyo yaliyotumiwa.

Polisi wa Indonesia akimbilia karibu na eneo la mlipuko.
Polisi wa Indonesia akimbilia karibu na eneo la mlipuko.

Haijajulikana bado nani alihusika na milipuko hiyo au ikiwa wamekamatwa au kuuliwa. Vyombo vya habari vya Indonesia vinaripoti kwamba kulikuwepo angalau wanamgambo 14 walohusika katika mashambulizi hayo.

Rais Joko Widodo akizungumza kwenye televisheni ya taifa alilaani "vitendo hivyo vya kigaidi", akisisitiza kwamba maafisa wa usalama wanafanya kazi kudhibiti hali ya mambo.

XS
SM
MD
LG