Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:29

Maalif Seif na CUF Zasisitiza Kutorudiwa Uchaguzi Zanzibar


Mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar umeingia katika hatua nyingine baada ya Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais wa chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kusisitiza hakubaliani na merejeo ya uchaguzi.

Seif alieleza hayo Jumatatu jijini Dar es Salaam alipofanya mkutano wake na wanahabari na kuweka bayana kwamba chama chake hakitarudia uchaguzi huo.

Maalim Seif Shariff Hamad ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika serikali ya umoja wa kitaifa baina ya CCM na CUF ameitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangza matokeo ya majimbo yaliyosalia.

Awali Seif alizungumzia kwa kina kiini cha mgogoro wa Kikatiba na Kisheria uliotokana na kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar, ambapo pia amebainisha namna ya kuutatua.

Amesisitiza kwamba kurejea uchaguzi wa Zanzibar bila ya kupata ufumbuzi juu ya uhalali wa uamuzi wa Mwenyekiti wa ZEC, ni sawa na kuhalalisha kitendo cha Mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Said Jecha, alifuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25 mwaka jana, kitendo ambacho Hamad amedai hakina mashiko ya kisheria wala Kikatiba.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:28 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG