Majasusi kutoka Kenya na Ufaransa wameungana kukagua kifaa kilichodai
kuwa bomu kilichokuwa ndani ya ndega ya abiria iliyotua kwa dharura
Jumapili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi mjini
Mombasa.
Ndege hiyo AF 463 aina ya Boeing 777 ya shirika la Air France ilikuwa
na abiria 459 na wahudumu 14 kutoka nchi ya Mauritius kueleka mjini
Paris,Ufaransa, lakini rubani akalazimika kuomba kutua katika uwanja
huo wa Moi ulio Mombasa katika pwani ya Kenya kutokana na hofu ya bomu
hilo.
Waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya Joseph Nkaissery Jumapili aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja huo kuwa majasusi wa kigeni na wenzao wa Kenya wameshirkiana kukagua mizigo
yote iliyokuwa ndani ya ndege hiyo.
Waziri huyo alidhibitsha kuwa abiria waliokuwa ndani ya ndega ya Air France wamepata hifadhi katika hoteli kadhaa katika mji wa Mombasa.
Watalii wengi pia walipata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu kwa
sabbau ya hofu kubwa iliyowakumba tangu wakiwa angani kutoka Mauritius
na hadi walipotua mjini Mombasa.
Idara ya polisi kupitia msemaji Charle Owino ilitoa taarifa hiyo muda
mfupi baadaye Jumapili, na kwamba ndege hiyo ilikuwa imeondoka
Mauritius Jumamosi usiku na kutarajiwa kutua Paris katika uwanja wa
Charles de Gaulle..
Mpaka kufikia Jumapili jioni ndege hiyo ilikuwa katika uwanja wa ndege, huku ukaguzi ukiendelea kuhusu madai ya kubeba bomu na abiria kadhaa wakiendelea kuhojiwa.
Ndege ya Ufaransa Yatua Mombasa kwa Hofu ya Bomu
