Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 05:35

Watu 59 Wapotea Katika Maporomoko ya Tope China


Vyombo vya habari vya China vinasema watu 59 bado hawajulikani walipo baada ya maporomo makubwa ya matope kupiga sehemu ya kusini mwa nchi hiyo.

Matope hayo yamezika majengo 22, yakiwemo mabweni mawili ya wafanyakazi wa viwandani.

Maafisa wanasema watu wanne wameokolewa kutoka kwenye vifusi, watatu kati yao wakiwa na majeraha madogo.

Shirika rasmi la habari la China limesema maporomo ya matope yalipiga eneo la Shenzhen katika jimbo la Guangdong Jumapili asubuhi.

Vilevile matope hayo yalifunika eneo zima na kuchochea bomba la gesi kulipuka katika eneo la jirani.

Zaidi ya wafanyakazi wa uokozi 1,500 wamepelekwa katika eneo hilo kuwatafuta watu walionusurika.

Takriba watu 900 wameondolewa kabla ya maporomoko ya matope kuanza.

XS
SM
MD
LG