Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 04:29

Serikali ya Niger Yazuia Mapinduzi


Serikali ya Niger imezima mpango wa mapinduzi na kusababisha watu kadhaa kukamatwa kwa mujibu wa Rais Mahamadou Issoufou.

Rais Issoufou alizungumza hayo alipokuwa akilihutubia taifa kwa njia ya radio na televisheni Alhamisi na kusema hali sasa ni shwari.

Tangazo hilo limekuja baada ya chombo kimoja cha habari nchini humo na taarifa katika mitandao ya kijamii siku ya Jumatatu kusema kwamba maafisa wanne wa ngazi ya juu wa jeshi wamekamatwa.

Pamoja na kuwwapo taarifa hizo za kukamatwa maafisa wa jeshi lakini taarifa hizo hazikuthibitishwa na mamlaka za Niger.

Rais Issoufou alisema kwamba serekali imefanikiwa kuzima jaribio la kutaka kudhoofisha taasisi zao.

Tangazo hilo limetoka katika usiku ambapo nchi hiyo inajiandaa kufanya sherehe za uhuru.

Hakukuwa na taarifa kutoka kwa upinzani kwa taifa hilo koloni la zamani la Ufaransa.

XS
SM
MD
LG