Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:05

Wavuvi waliokamatwa Mombasa waachiwa kwa dhamana.


Boti ya wavuvi kutoka Zanzibar.

Mahakama ya Kilifi nchini Kenya Jumanne imewaachia kwa dhamana wavuvi 95 kutoka Pemba waliokamatwa baharini kwa madai ya kuvua katika himaya ya Kenya bila idhini kutoka idara ya uhamiaji.

Walishitakiwa katika mahakama mbili tofauti kwa makosa ya kuingia Kenya kimyume cha sheria na kufanya shughuli za uvuvi bila kibali baada ya kuzuiwa na maafisa wa usalama kwa siku tatu.

“Tulikuwa tunataka serikali ya Kenya iangalie zaidi sheria sio mabavu kwasababu hawa walioshikwa wote wameingia Kenya kihalali kabisa” alisema mmoja wa wavuvi kutoka Pemba Tanzania Kombo Shekha Kombo.

Hata hivyo mashtaka hayo yameibua hisia kali miongoni mwa vyama vya wavuvi kutoka Kenya na Tanzania, wakisema kwa miaka mingi wamekuwa baharini kuvua bila kujali mipaka ya bahari Afrika Mashariki.

XS
SM
MD
LG