Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:22

Mataifa Makubwa Yakamilisha Mazungumzo Libya


Maafisa wa serikali zinazopingana nchini Libya wakiwa katika moja ya mikutano ya mgogoro wa Libya.
Maafisa wa serikali zinazopingana nchini Libya wakiwa katika moja ya mikutano ya mgogoro wa Libya.

Mataifa yenye nguvu duniani yamekamilisha mkutano na wawakilishi wa pande mbili zinazopingana na kuhasimiana nchini Libya.

Pia mataifa hayo yametoa uhakika wa kusaidi mpango unaungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambao utaanzisha serikali ya umoja wa kitaifa.

Wawakilishi wa nchi 17 na vyombo vinne vya dunia walifanya mkutano na maafisa wa Libya mjini Rome, Italia Jumapili katika mkutano ambao uliongozwa na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwezake wa Italia, Paolo Gentiloni.

Mkutano huo umefanyika wakati pande mbili za Libya zinajiandaa kutia saini makubaliano ya umoja wa kitaifa katika ghafla itakayofanyika nchini Morocco Jumatano.

Libya imekuwa katika machafuko toka serikali iliyokuwa ikiongozwa na kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi kuangushwa.

XS
SM
MD
LG