Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:31

China Yandaiwa Kuendelea Kufanya Mateso


Tunisian protesters throw stones towards security forces in Tunis' Djebel Lahmer district after price hikes ignited protests in the North African country.
Tunisian protesters throw stones towards security forces in Tunis' Djebel Lahmer district after price hikes ignited protests in the North African country.

Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya mateso imesema mateso na vitendo vibaya vimesambaa nchini China.

Vitendo hivi vimepigwa marufuku kimataifa vimeendelea kushamiri katika mfumo wa kisheria wa nchi hiyo.

Kundi la wataalamu 10 wa kujitegemea wanasema ujumbe wa China ambao uliwasilisha kesi yake kwa kamati ya Umoja wa Mataifa na kukiri kwamba mateso ni tatizo kubwa nchini China.

Kamati hiyo inasema ujumbe wa China haukutoa takwimu za kiwango cha vitendo hivyo vilivyopigwa marufuku.

Jopo limesema unjumbe wa China pia haukuweza kutoa taarifa za idadi ya watu walifoariki wakiwa chini ya ulinzi.

Vilevile haikutoa taarifa watu wangapi wanashikiliwa bila ya kuwa na mawasiliaono katika sehemu za siri za kushikilia watu zinazojulikana kama “jela nyeusi” pamoja na kesi ngapi za mateso zimewasilishwa na kufanyiwa uchunguzi.

Kwa mujibu wa kanuni za Umoja wa Mataifa nchi zilizo chini ya uangalizi lazima zijibu maswali na wasiwasi unaoelezewa na kamati ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

China haijajibu nasuala yaliyoulizwa mwaka 2008 na bado hayaja-tatatuliwa.

Mwanakamati hiyo, Jens Mosvig ameiambia VOA kwamba matatizo haya yanahusiana na shutuma za ukamataji wanaofanyiwa wanasheria na watetezi wa haki za binadamu.

“Ishara ya kusambaa kwa tatizo hili la mateso ni matumizi ya kile kinachoitwa viti vya mahojiano, ambapo viti hivyo vimechimbiwa ardhini na na watu wanaofanyiwa mahojiano hufungwa mikono na hakuna kiwango cha muda wa mahojiano yanayofanyika.” Alisema Mosvig

Modvig anasema aina hii ya vitendo ambayo kwa urahisi vinaweza kuelezewa ni mateso ni aina ya mbinu za mahojiano ambazo zimeagizwa.

Kamati ya Umoja wa Mataifa imeelezea kusikitishwa kwake kuhusu kuwekwa kizuizini kwa watu na kuhojiwa kwa zaidi ya wanasheria 200 na wanaharakati tangu mwezi Julai.

Kamati ina hofu manyanyaso kama haya na masharti mengine yanaweza kuwazuia wanasheria kuwasilisha ripoti ya mateso wanayowapata wateja wao kwa hofu ya kufanyiwa vitendo visivyo haki.

Mwaka 2013, mahakama kuu ya China ilipiga marufuku mateso na kutaka kufanyika kwa mageuzi ya sheria ya jinai lakini makundi ya haki za binadamu yanasema vitendo vya mateso bado vinaendelea kutumika.

XS
SM
MD
LG