Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:08

Power: Rais Kagame Atakiwa Kuachia Madaraka 2017


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power, ametoa mwito kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuheshimu utaratibu wa muhula wa kukaa madarakini.

Bi Power ametaka Rais Kagame kuachia madarakani itakapofika mwisho wa mwaka 2017.

Samantha Power aliongea hayo na wanahabari wakati wa kuanza uongozi wa Marekani katika baraza la usalama la Umoja wa Mtaifa Jumanne.

Amesema baraza la usalama linafikiria kutembelea nchini Burundi ambapo kuna mgogoro wa kisiasa uliosababisha vifo vya watu kadhaa kutokana na muhula wa tatu ulio nje ya katiba wa Rais Pierre Nkurunziza.

Amesama hatua ya baadhi ya viongozi wa kiafrika kuongeza muda wa kukaa madarakani na kupuuzia ukomo wa mihula ni hatua mbaya inyoshika kasi.

Power amesema anamatumaini Rais Paul Kagame wa Rwanda atatumia fursa na kuwa mfano katika ukanda huo kwa kuachia madaraka kwa amani.

XS
SM
MD
LG