Papa Francis ametoa wito wa umoja na maridhiano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuwataka wananchi kutoruhusu tofauti za kidini kuwagawanya, anapokamilisha ziara yake ya kwanza Afrika.
Hii ni mara ya kwanza katika historia kwa kiongozi wa kanisa la Katholiki katika nchi inayokumbwa na ghasia, ziara ianyofanyika chini ya ulinzi mkali wa majeshi ya kimataifa.
Katika hotuba aliyotoa ikulu ya Bangui, Papa Francis amesema, ana matumiani uchaguzi wa mapema mwanaki utairuhusu nchi hiyo kuanza ukurasa mpya msafi katika historia yake.
Kabla ya kuwasili kwake kaimu Rais Catherine Samba-Panza, aliwambia wananchi siku ya Jumamosi kuchukulia ziara ya Papa Francis kua ni ujumbe wa Amani.
Anasema wananchi wengi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wana matumiani ujumbe atakayoutoa utaleta hisia ya kuwapa watu hamasa ya kujifunza namna ya kukubaliana na kuweka kando tofauti zao na kuishi tena kwa pamoja na kuendelea mbele kwa Amani.