Upatikanaji viungo

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amedai kwamba wapinzani wake wakuu wana njama za kuharibu jeshi la Uganda na kutaka kumuondoa madarakani.

Bwana Museveni aliyazungumza hayo katika mkutano na wanahabari ambapo katika mkutano huo amewalenga Amama Mbabazi, na Kiiza Besigye.

Vilevile Rais Museveni katika shutuma zake alimtaja aliyekuwa kiongozi wa ujasusi katika jeshi la Uganda, Generali David Sejusa.

Amesisitiza kwamba aliwapa viongozi hao wa zamani wa serikali na jeshi la Uganda nafasi ya kutatua matatizo ya nchi na wakashindwa kuyatekeleza.

Amedai yale yanayozungumzwa na wapinzani wake ni porojo kwa wapiga kura wakiwa na lengo la kumuondoa madarakani kwa kulitumia jeshi.

Uganda itafanya uchaguzi wake mwakani mwezi Febuari, ambapo katika kiti cha urais, wamejitokeza wagombea wanane lakini vinara ni Rais Museveni mwenyeye, Kiiza Besigye na Amama Mbabazi.

XS
SM
MD
LG