Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 10:59

UKAWA wahoji uhalali wa Magufuli kuhutubia bunge


Bunge la Tanzania

Kambi ya upinzani na wabunge wanaounda umoja wa UKAWA wamemwandikia barua spika wa Bunge la Tanzania wakitaka ufafanuzi wa katiba ili kujua kama Rais John Pombe Magufuli ana haki ya kufungua Bunge.

Akiongea na VOA Swahili mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia amesema haileti maana kwa Rais huyo wa Tanzania kuhutubia Bunge wakati mpaka sasa ni kama hakuna Rais wa Zanzibar, baada ya uchaguzi wake kufutwa.

Vile vile Mbatia amesema, ushindi wa Rais Magufuli pia una mashaka kwa kuwa upande mmoja wa Tanzania, yaani Zanzibar uchaguzi wake umefutwa kitu ambacho amekieleza kama kutokamilisha maana ya muungano.

Katika mazungumzo hayo Mbatia hakuweka wazi ni nini hasa ambacho wanatarajia kufanya wao kama UKAWA endapo Rais Magufuli atakwenda Bungeni na kutoa hotuba yake.

Rais John Pombe Magufuli anatarajia kulihutubia Bunge la 11 la Tanzania siku ya Ijumaa, mara baada ya Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo atakapo tangazwa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:07 0:00
Kiungo cha moja kwa moja
XS
SM
MD
LG