Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:07

Jumuiya ya Kimataifa yaitaka Burundi kuanzisha Mazungumzo ya Kitaifa


Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza.

Maafisa wa Uganda wamesema Ijumaa kwamba mwakilishi mmoja wa Marekani yupo nchini Uganda kuhamasisha mazungumzo ya kutatua matatizo ya kisiasa nchini Burundi kama ambavyo jumuiya ya kimataifa inavyosihi kuwepo mashauriano bila ya masharti yeyote.

Tom Perriello, mwakilishi wa Marekani kwa ajili ya nchi za kanda ya maziwa makuu anaitembelea Uganda kushauriana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni juu ya namna ya kuanza tena mashauriano ya Burundi, alisema Okello Oryem, naibu waziri wa mambo ya nje wa Uganda.

"Majaribio ya awali kwenye mashauriano yalionekana kuwepo na upungufu wa ushirikiano na hatua za taratibu kutoka pande zote zinazohusika nchini Burundi," alisema Oryem.

Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Uganda Okello Oryem
Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Uganda Okello Oryem

Wakati huo wajumbe wa Umoja wa Afrika wamekutana Ijumaa mjini Addis Ababa kuzungumzia juhudi za kikanda na kimataifa juu ya kutanzua ugomvi huo wa Burundi.

Siku ya Alhamisi

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa wito kwa vyama vinavyopigana nchini Burunsi kusitisha ghasia na kutatua masuala yao kupitia majadiliano. Wanachama wote 15 walipiga kura kuidhinisha azimio ambalo litazuia mali na kuweka marufuku ya safari kwa watu ambao wanazuia Amani na kuchochea ghasia.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Azimio hilo pia linaidhinisha kupelekwa kwa waatalamu wa sera na usalama ili kutathmini kile kinachohitajika kuwasaidia watu wa Burundi. Ghasia ziliibuka nchini Burundi mwezi April wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza uamuzi wake wa kuwania awamu ya tatu madarakani, hatua ambayo upinzani iliita ni kinyume cha katiba.

Marekani, umoja wa ulaya na majirani wa taifa hilo lililopo Afrika mashariki wanakhofu ghasia zitaweza kupelekea vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

XS
SM
MD
LG