Pamoja na Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein, kuzidisha kipindi cha muhula wake wa kwanza kutokana na mgogoro wa kisiasa inaelezwa bado anatambulika kama rais mwenye mamlaka yote.
Kwa mujibu wa mtaalamu wa sheria Dkt Damas Ndumbaro, wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, aliyezungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, amesema kwa sasa Rais Shein ni halali kuendelea Zanzibar.
Dkt Ndumbaro ameongeza kwamba, hakuna kipengele cha sheria ambacho kinatamka kuundwa kwa kamati ama chombo kitacho ongoza visiwa vya Zanzibar kwa kipindi kama hiki.
Mpaka sasa kuna hali ya sintofahamu inayoendelea visiwani humo, mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha kufuta uchaguzi wa Oktoba 25.
Unaweza kusikiliza mahojiano hayo ya Dkt Damas Ndumbaro na Idhaa hii hapo chini.