Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:41

Ndege za Russia Zasimamishwa Kwenda Misri


Rais wa Russia Vladimir Putin aliyesitisha ndege za Russia kwenda Misri.

Rais wa Russia amesimamisha safari zote za ndege za kibiashara kwenda Misri Ijumaa.

Hilo limetokea wakati wachunguzi wakiendelea kuchunguza kama bomu liliangusha ndege ya Russia mwishoni mwa juma lililopita.

Ndege ya shirika la Russia la Metrojet aina ya Airbus A 321ilianguka kwenye Peninsula ya Sinai na kuuwa watu 224 waliopanda ndege hiyo.

Kiongozi huyo wa Russia alichukua hatua ya haraka baada ya mkuu wa idara ya usalama ya nchi hiyo Alexander Bortnikov kupendekeza hivyo.

Bartnikov alitaka kusimamishwa kwa safari hizo mpaka tutakapojua sababu maalum kwa ajali hiyo ya Jumamosi.

XS
SM
MD
LG