Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:24

Kenya yajiandaa kumpokea Papa Francis.


 Papa Francis na Naim Ternava
Papa Francis na Naim Ternava

Shamra Shamra za kumpokea Papa Francis kiongozi wa kanisa katoliki duniani zimeanza kushika kasi nchini Kenya huku viongozi wa dini mbali mbali wakitoa ujumbe wa kumkaribisha papa huyo.

Katika eneo la pwani ya Kenya madhehebu mbali mbali yanatumia fursa hiyo kuhimiza amani na utengamano kati ya dini mbali mbali.

Takriban waumini 2000 wa kikatoliki kutoka Mombasa wanajiandaa kwenda mji mkuu wa Nairobi, kwa ajili ya kumkaribisha Papa Francis anayetarajiwa kutembelea nchini Kenya mwishoni mwa Novemba.

Kiongozi wa kanisa hilo parokia ya Mombasa Wilberd Largo anasema kabla ya kwenda huko watandaa maandamano ya amani yatakayohusisha dini mbali mbali ikiwa ni pamoja na wakristo, wahindu na waislam ili kuhimiza amani na utangamano.

XS
SM
MD
LG