Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 15:56

Wakenya wawika tena mbio za marathon New York


Kundi la wanaume wanaoongoza mbiyo za marathon za New York 2015

Mary Keitany wa Kenya, kwa mwaka wa pili mfululizo amemaliza mbiyo mashuhuri za Marathon za New York kwa ushindi, lakini sio sawa na alivyofanya mwaka jana.

Mary Keitany akivuka utepe wa kumaliza mbiyo za New York 2015
Mary Keitany akivuka utepe wa kumaliza mbiyo za New York 2015

Mama huyo mwenye umri wa miaka 33 akiwa na watoto wawili ni mwanamke wa pili kushindi mbiyo za New York Marathon kwa miaka miwili mfululizo. Mara ya mwisho kwa mwanamke mwengine kufanya hivyo ilikua mwaka 2007 na 2008, pale Muingereza Paula Radcliffe kufanya hivyo.

Kwa upande wa wanaume Stanley Biwott, mwenye umri wa miaka 29, alinyakua ushindi wake wa kwa wa mbiyo za kimataifa za marathon akitumia muda wa saa 2 dakika 10 na sekunde 34.

Stanley Biwott wa Kenya akiongoza kundi la wanaume katika mbiyo za marathon za New York
Stanley Biwott wa Kenya akiongoza kundi la wanaume katika mbiyo za marathon za New York

Biwott alimzuia Mkenya mwenzake Wilson Kipsang kunyakua taji la ushindi wa pili mfululizo wa mbiyo hizo za 45 za New York na kumshinda mwenzake Geoffery Kamworor aliyechukua nafasi ya pili akiwa sekunde 14 nyuma.

Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Wakenya kunyakua ushindi wa wanaume na wanawake katika mbiyo za New York.

XS
SM
MD
LG