Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:43

Al-Shabab Yadai Kuhusika na Shambulio la Hoteli Sahafi


Mpigaji picha wa Reuters Feisal Omar, kati, alijeruhiwa na mlipuko wa bomu akiwa na jamaa zake nje ya hospitali ya Medina Hospital Mogadishu, Somalia, Nov. 1, 2015.
Mpigaji picha wa Reuters Feisal Omar, kati, alijeruhiwa na mlipuko wa bomu akiwa na jamaa zake nje ya hospitali ya Medina Hospital Mogadishu, Somalia, Nov. 1, 2015.

Waziri wa Usalama wa Somalia Abdirizak Omar Mohamed ameiambia Sauti ya Amerika kwamba, washambulizi watano au sita wa Al-Shabab walishambulia Hoteli ya Sahafi mjini Mogadishu baada ya mabomu mawili yaliyotegwa ndani ya gari kulipuliwa na wajitoa mhanga mbele ya mlango wa kuingia ndani ya hoteli. Wapiganaji hao, anasema walishindwa nguvu baada ya mapigano na vikosi vya usalama.

Mmoja kati ya aliyeuliwa alikua mkuu wa zamani wa jeshi la Somalia, Jenerali Abdulkarim Yusuf ambae amenusurika majaribio kadha ya mauwaji na kupigana vikali dhidi ya kundi hilo la kigaidi alipokua madarakani.

Hoteli Sahafi iliyoshambuliwa na Al-Shabab
Hoteli Sahafi iliyoshambuliwa na Al-Shabab

Maafisa wa usalama wanasema, wanamgambo walilipua mabomu hayo yaliyotegwa ndani ya gari mapema asubuhi, na hapo tena washambulizi walokua na bunduki walivamia hoteli hiyo mashuhuri inayotembelewa sana na maafisa wa serikali na wafanya biashara. Mashahidi wanasema wasilikia milio ya bunduki kwa muda mrefu ndani ya hoteli hiyo.

Meja wa polisi Ismail Nur ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba polisi waliwaokowa maafisa wengi wa serikali kwa kuweka ngazi katika ukuta wa nyuma wa hoteli. Nur anasema polisi walipigiwa simu na wafanyakazi walokua wanajificha ndani ya jengo hilo wakisema kuna watu walojeruhiwa wakiwemo maafisa wa serikali ndani ya hoteli hiyo.

Nyumba ya watu walokua karibu na hoteli imeharibiwa na mlipuko
Nyumba ya watu walokua karibu na hoteli imeharibiwa na mlipuko

Wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM, na vikosi vya usalama vya Somalia hatimae walifanikiwa kuchukua udhibiti wa hoteli hiyo, saa chache baadae.

Katika mieizi ya hivi karibuni wapiganaji wa Al-Shabab wamefanikiwa kushmabulia hoteli nyingine mjini Mogadishu, kuvamia na kuchukua udhibiti wa muda wa kambi tatu za AMISOM huko Somalia na kulipua bomu katika uwa wa Ikulu ya rais huko Mogadishu.

Kundi hilo liliondolewa kutoka ngome zake za kusini mwa nchi mwaka 2010 na wanajeshi wa serikali na AMISOM, lakini kukimbilia maeneo ya mashambani. wanamgambo hao hivi sasa wanafanya mashambulio ya hapa na pale kwa kuwalenga maafisa wa serikali na wanajeshi wa AMISOM.

XS
SM
MD
LG