Wagombea 10 wa juu wanaopigania kuchaguliwa kuwa mgombea kiti cha rais kwa niaba ya chama cha Republikan, walipambana Jumatano usiku juu ya sera zao za kiuchumi na kushambuliana juu ya masuala mbali mbali wakati wa mdahalo wao wa tatu.
Mdahalo huo ulodhaminiwa na kituo cha Televisheni cha CNBC umefanyika wakati bilionea Donald Trump anaonekana kupoteza nafasi ya juu ya umashuhuri, aliyokua anashikilia kwa miezi kadhaa sasa katika kinyan’gnanyiro cha warepublican.
Trump mtu asiyeogopa kusema anachofikiri na ambaye kwa sasa yuko nyuma ya Daktari wa upasuaji wa kichwa Ben Carson katika uchunguzi kadhaa wa maoni, alionekana akiwa hana nguvu kubwa ikilinganishwa na midahalo mingine.