Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:51

NEC imeanza kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa Tanzania


Maafisa wa NEC wakihesabu kura wakiangaliwa na wawakilishi wa vyama vuya kisiasa
Maafisa wa NEC wakihesabu kura wakiangaliwa na wawakilishi wa vyama vuya kisiasa

Tume ya uchaguzi ya taifa ya Tanzania NEC, imeanza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi kama ilivyoahidi mapema, huku baadhi ya wapiga kura wa Dar es Salaam watazamia kupiga kura.

Mwenyekiti wa NEC Jaji aliyestahafu Damian Lubuva alitoa matokeo ya majimbo matatu ya uchaguzi ambapo mgombea kiti wa chama tawala CCM John Magufulu anaongoza.

Jaji Lubuva amesema matokeo zaidi yatatolewa wakati wa saa sita mchana.

Huko Zanzibar tume ya uchaguzi imetangaza pia matokeo ya majimbo matatu, na matokeo hayo ya awali yana mweka mbele mgombea kiti wa chama tawala cha CCM Ali Mohamed Shein

Waandishi wa Sauti ya huko Dar es Salaam na Zanzibar wanaripoti kwamba ni mapema mno kuweza kusema nani ataweza kupata ushindi na wanaripoti kwamba hali inaendelea kuwa shuwari huku watu wakisubiri kwa hamu matokeo ambapo kuna wengi hawakulala wakitaka kuhakiisha kura zinahesabiwa kwa njia ya haki.

XS
SM
MD
LG