Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 08:31

Vituo vya kupigia kura Tanzania vyafungwa


Watanzania waiga foleni kuchagua Rais, Wabunge an Madiwani
Watanzania waiga foleni kuchagua Rais, Wabunge an Madiwani

Vingi vya vituo vya kupigia kura vimefungwa baada ya muda rasmi wa zoezi hilo kuyoyoma. Watanzania walionekana kupiga foleni Kuwachagua iongozi wao wa Kisiasa kwenye zoezi ambalo limetajwa na baadhi ya waangalizi kama tulivu na lenye amani.

Baadhi ya vituo vya kupigia kura vimefungwa baada ya muda uliowekwa wa zoezi hilo kuyoyoma huku Watanzania wakisubiri kwa hamu kujua ni nani aliyeibuka mshindi katika uchaguzi wa kitaifa na ule wa kisiwa cha Zanzibar mwaka huu.

Watanzania leo Jumapili wamejitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi, wengi wao wakipigiga foleni mapema kabla ya shughuli ya kupiga kura kuanza.

Baadhi ya walihojiwa wamesema kwamba wanatarajia mabadiliko yalioahidiwa na chama cha upinzani cha Chadema, huku wengine wakiwa wamerithika na kazi ya Chama tawala cha CCM.

Barabara nyingi mjini Dar es Salaam ambazo kwa kawaida huwa zenye shughuli nyingi zilikuwa tulivu kutokana na magari kuzuiwa kuingia mjini.

Wapiga kura walijitokeza kwenye vituo vya kupigia kura kote mjini hata kabla ya saa moja wakati uliowekwa wa kuanza zoezi hilo.

Hali ilikua ni hiyo hiyo katika kiziwa cha Zanzibar ambako uchaguzi wa Rais na makamu wake.

Hata hivyo, kumekuwa na ripoti za hali ya taharuki katika baadhi ya vituo vya kupigia kura kutokana na ukosefu au kasoro kwenye makaratasi ya kupigia kura lakini waangalizi wa nchini, wale wa kimataifa pamoja na wawakilishi wa vyama vya kisiasa nchini walionekana kukubaliana kwa kauli moja kwamba, kwa ujumla zoezi hilo liliendeshwa kwa utulivu na amani.

XS
SM
MD
LG