Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:03

Uganda yaondoa wanajeshi kwa hiari Sudan Kusini.


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akiwapungia mkono wananchi.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akiwapungia mkono wananchi.

Msemaji wa rais wa Uganda Ateny Wek Ateny anasema, Kuondolewa kwa hiyari wanajeshi wa Uganda kutoka Sudan Kusini, ni ishara ya dhamira ya dhati ya serikali kutekeleza kikamilifu makubaliano ya amani yaliotiwa saini baina ya Rais Salva Kiir na Makamu Rais wa zamani wa Sudan Kusini, Riek Machar. Bw. Ateny, anasema zoezi zima la kuwaondoa wanajeshi litakamilika wiki ya kwanza ya Novemba.

Kuondolewa kwa wanajeshi wa Uganda ni moja wapo ya matakwa makuu ya waasi watiifu kwa makamu rais wa zamani wa Sudan Kusini, Riek Machar, wakati wa majadiliano ya amani ili kumaliza mzozo wa taifa hilo yalofanywa mjini Addis Ababa.

Serikali ilikataa matakwa ya waasi, ikieleza kuwepo na makubaliano baina ya serikali na serikali kati ya utawala wa Juba na Kampala yalopelekea kuweko kwa vikosi vya Uganda huko Sudan Kusini.

Ateny anasema rais Kiir ameonyesha utashi wa kisiasa wa kutaka kurejesha Amani nchini mwake.

“Huu ni utaratibu ambao ulikuliwa ndani ya makubaliano ya kutanzua mzozo wa Sudan Kusini, ambayo yanewataka wanajeshi wa Uganda na wanajeshi wengine wowote kuondoka Sudan Kusini." alisema Ateny.

Hata hivyo kutakuwepo na wanajeshi wa jeshi la UPDF katika jimbo la Equitorial ya magharibi la Sudan Kusini, ambako wamewekwa kuwasaka na kukabiliana na waasi wa Lords resistance army LRA.

Makundi ya upinzani na waasi watiifu kwa Machar wanasema kuondolewa kwa wanajeshi wa UPDF kutasaidia sana utekelezaji wa mkataba wa amani.

Makubaliano yanolengwa kurudisha amani kwa taifa hilo kufwatia mzozo ambao umepelekea takriban watu millioni mbili kupoteza makazi yao.

Bw. Ateny anasema waasi watabidi kuonyesha dhamira yao ya dhati ya kutekeleza makubaliano ya amani.

Anasema watu wa Sudan kusini wako tayari kuhakikisha kuwa makubaliano ya amani yanatekelezwa kwa ukamilifu na pande zote.

Hata hivyo, serikali na waasi wanaendelea kubadilishana malalamiko kuhusu ukiukaji wa mkataba ulotiwa saini hivi karibuni.

Mashirika ya kutowa misaada yalielezea wasiwasi kuwa mzozo unaoendelea katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo unasababisha hali kuwa ngumu kutoa msaada unaohitajika kwa raia wanojikuta katikati ya mapambano. Ateny anasema serikali itatoa ulinzi kwa wafanyaazi wa kutoa misaada katika maeneo ambayo vikosi vya kitaifa vinadhibiti.



XS
SM
MD
LG