Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 23:19

Vyuo vikuu zaidi ya 10 vyafungwa kwa muda Afrika Kusini


Makundi ya watu wakiandamana Johannesburg, South Africa.
Makundi ya watu wakiandamana Johannesburg, South Africa.

Karibu vyuo vikuu 14 vya Afrika kusini vimefungwa kwa muda wakati wa kuongezeka kwa wimbi la malalamiko na maandamano ya wanafunzi kutokana na mapendekezo ya kuongezwa kwa ada. Maandamano hayo yamepelekea mapambano Jumatano kati ya wanafunzi na polisi nje ya bunge huko Capetown.

Malalamiko yalianza wiki iliyopita katika chuo kikuu cha Witwatersrand huko Johannesburg baada ya mapendekezo ya ongezeko la asilimia 10. Toka wakati huo ujumbe wa Twitter “ada lazima ipungue”umesambaa kwenye mitandao ya kijamii na malalamiko yametapakaa katika taasisi tofauti ikiwa ni pamoja na chuo kikuu mashuhuri cha Capetown, chuo kidogo cha kiliberali Rhodes na kile cha nje ya mji Fort Hare.

Maandamano hayo yamelazimisha viongozi wa vyuo vikuu kukutana wiki hii na waziri wa elimu ya juu na mafunzo Blade Nzimande katika jaribio la kutafuta suluhu.

XS
SM
MD
LG