Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:46

Mbowe anasema CHADEMA hakitofanya fujo wakati na baada ya uchaguzi


Mkutano mkuu wa UKAWA Jangwani Dar es Salaam
Mkutano mkuu wa UKAWA Jangwani Dar es Salaam

Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema, Freeman Mbowe amesema wamepokea kwa mshangao na masikito kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu hoja ya kukaa mita 200 kutoka eneo la kupigia kura .

Alisema "mwenye haki ya kuzungumzia na mamlaka, si Rais Kikwete bali ni tume ya uchaguzi ya Tanzania na wamekuwa wakisema tume hiyo ina haki ya kuwa huru na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na si kwa maelekezo ya rais."

Bw Mbowee anadai kwamba kitendo hicho cha rais ni kuvunja sheria na haki.

Bendera za vyama vya kisiasa katika barabara kuelekea Jangwani Dar es Salaam
Bendera za vyama vya kisiasa katika barabara kuelekea Jangwani Dar es Salaam

Rais Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba, wapiga kura wasikae mita 200 karibu na vituo vya kupiga kura bali waende majumbani baada ya kupiga kura hapo Oktoba 25.

Mbowe aliongeza kueleza kwamba agizo la kuwataka watu hao wapige kura na kurudi nyumbani kulala la sivyo watashughulikiwa na vyombo vya dola si utawala bora.

Akijibu swali kuhusu amani na kuwandaa kisaikojia wanachama kuendelea kuwa watulivu bila kujali nani anashinda, Mbowe alisema, "amani ni muhimu kuliko jambo lolote katika nchi, lakini amani haitapatikani kwa kuvunja sheria na amani hatapatikana kwa woga ila amani itapatikana pale haki itakapotamalaki na utawala wa sheria utakapochukua nafasi yake."

Kiongozi huyo wa upinzani, aliongeza kwa kusema “Chadema hatukusudii kufanya fujo, hatuna sababu ya kufanya fujo kwasababu tunashinda ila tunataka watanzania wasijengwe na nidhamu ya woga tunavitaka vyombo vyote vya dola na wadau wengine wote wanaohusika na masuala ya haki katika mchakato mzima wa uchaguzi huu wahakikishe kwamba haki ipatikane na ionekane inapatikana.”

Lakini akaonya kama watatumia mamlaka yao vibaya na kuwaonea wananchi , basi hiyo amani inaweza isipatikane .

Aidha alitoa rai kwa Rais Kikwete asihutubie taifa usiku wa mkesha wa kupiga kura kwani suala hilo linaweza kuyumbisha taifa, akitolea mfano kwamba haijawahi kutoka kwa marais wote waliomtangulia nchini humo kufanya hivyo.

Alitolea mfano hotuba aliyotoa wakati wa bunge maalum la katiba, anasema “alivuruga hali ya mambo mpaka taifa likakosa katiba mpya.”

Mahojiano na Mbowe
please wait

No media source currently available

0:00 0:06:33 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizungumzia juu ya ikiwa mgombea wa Ukawa atajiandaa na hotuba mbili ya kushinda na kushindwa, alisema, utafiti unawaonyesha wanashinda kwa zaidi ya asilimia 78, ila hata kama ikitokea wakashindwa ataongea maneno matatu tu na “ hiyo itakuwa ni miujiza” kwa wao kushindwa.

Lowassa anatarajiwa kupiga kura yake huko jimboni kwake Monduli alieleza.

XS
SM
MD
LG