Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:15

Wakenya Kipyego na Chepkirui watamba katika mbio za Amsterdam.


Bernard Kipyego kutoka Kenya ashinda mbiyo za Marathon za Amsterdam 2015.
Bernard Kipyego kutoka Kenya ashinda mbiyo za Marathon za Amsterdam 2015.

Kenya imetamba tena huko Amsterdam baada ya wanariadha wake Bernard Kipyego aliyetetea taji lake na Joyce Chepkirui kushinda katika mbio mashuhuri za Marathon za Amsterdam Jumapili.

Kipyego ambaye anatokea Metkei huko Keiyo Kusini ameshinda kwa kuvunja rekodi yake binafsi kwa kutumia saa mbili, dakika 6 na sekunde 18.

Kipyego mwanariadha mwenye kuona haya ameimarisha rekodi yake kwa sekunde 7, aliyoiweka mara ya mwisho 2011 katika mbiy za marathon za Chicago, Marekani.

Hali ya hewa iliyokuwa ya manyunu ya mvua na unyevu nyevu haikuwa nzuri kwa mbio hizo, hata hivyo wanariadha wote wawili waliweka rekodi ya muda wa kasi wa mara ya sita katika historia ya mbio hizo.

Wakimbiaji mashuhuri watatu Goeffrey Kirui, Edwin Kiptoo na Nicholas Bor, walijaribu kuongeza kasi za mbio hizo kwa lengo la kuvunja rekodi ya mbio hizo zilizowekwa na Wilson Chebet ya 2:05:27 aliyoweka 2011. Lakini kilometa chache baadaye wakimbiaji hao wa Kenya hawakufua dafu kwani waliishiwa nguvu, na kuona nafasi zao kuchukuliwa na Waethopia Chala Dechasa na Tsegaye Mekonnen.

Haikupita muda katika kilometa 30 Kipyego alichukua uongozi hadi ushindi akifuatwa na Wakenya wenzake Ezekiel Chebii na Mike Kigen.

Kwa upande wa wanawake Chepkirui mwenye umri wa miaka 27 kutoka Kericho County alishinda kwa kutumia saa 2 dakika 24 na sekunde 10, ikiwa ni mara yake ya tano kujaribu kunyakua ubingwa huo.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Mkenya mwenzake Flomena Cheyech aliyetumia muda wa 2:24:38, na nafasi ya tatu ikachukuliwa na mwanariadha kutoka Australia Milly Clark.

XS
SM
MD
LG