Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 02:57

Oscar Pistorius kuhamishiwa kifungo cha nyumbani.


Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akisindikizwa na Polisi baada ya kuhukumiwa Pretoria, Okt. 21, 2014.
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akisindikizwa na Polisi baada ya kuhukumiwa Pretoria, Okt. 21, 2014.

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius atatoka jela wiki ijayo na kuhamishiwa kwenye kifungo cha nyumbani, mwaka mmoja baada ya kuhukumiwa kumuuwa rafiki yake wa kike.

Idara ya magereza ya Afrika Kusini ilisema alhamisi kwamba Pistorius atahamishwa Oktoba 20 na kuwa kwenye kifungo cha nyumbani kwa miaka iliyobaki ya kifungo chake cha miaka mitano.

Pistorius alihukumiwa mwaka jana kwa kumpiga risasi na kumuuwa mwanamitindo Reeva Steenkamp nyumbani kwake Pretoria Februari 2013. Baraza la kutowa msamaha ilieleza jana kwamba Pistorius atabaki chini ya usimamizi wa magereza hadi oktoba 20 2019.

XS
SM
MD
LG