Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 20:55

Mrepublikan McCarthy hatogombania kiti cha spika


Kiongozi wa walio wengi bungeni Kevin McCarthy akiwa na spika anayestaafu John Boehner wakati mkutano huko Capitol Hill in Washington, Oktoba. 7, 2015.
Kiongozi wa walio wengi bungeni Kevin McCarthy akiwa na spika anayestaafu John Boehner wakati mkutano huko Capitol Hill in Washington, Oktoba. 7, 2015.

Mrepublikan aliyekuwa akitarajiwa sana kuchukua nafasi ya spika wa baraza la Wawakilishi katika bunge la Marekani aliwashtusha wenzake Alhamisi kwa kutangaza kwamba anajitoa kugombea nafasi hiyo.

Uamuzi wa kiongozi huyo wa walio wengi bungeni Kevin McCarthy unamaanisha mchuano wa kumtafuta spika wa bunge mpya kuchukua nafasi ya John Boehner uko wazi na utakua na ushindani mkubwa.

Kiongozi wa waliowengi. Kevin McCarthy,
Kiongozi wa waliowengi. Kevin McCarthy,

McCarthy amesema itabidi mtu mwingine ajaribu kusuluhisha mgawanyiko uliopo kati ya wahafidhina wa msimamo mkali na wahafidhina wa wastani wa chama hicho tawala bungeni

Anasema “na ninafikiri kuna kitu inabidi kisemwe, ili tuweze kuungana, kwa kweli tunahitaji mtu mpya. Nitaendelea kuwa kiongozi wa walio wengi, lakini kitu kimoja nilichogundua kwa kuongea na kila mtu ni kwamba kama tukiungana na kuwa wenye nguvu , tunahitaji sura mpya ili kusaidia hilo.”

Kati ya wale wanaotaka kugombea nafasi ya spika ni mjumbe wa baraza la Congress Jason Chafetz wa Utah.

Mshtuko huo ulifika nchi nzima mpaka Las Vegas ambako mgombea wa chama cha Republikan Donald Trump alitoa habari hiyo kwenye mkutano wa kisiasa.

Wa-Democrats pia walishangazwa na kufuatilia kwa karibu mgongano kwenye bunge. Msemaji wa White House

Josh Earnest, msemaji wa White House
Josh Earnest, msemaji wa White House

:

Amesema " kumekuwa na mpasuko kwenye chama cha Republikan inazungumzwa kwenye mikutano ya hadhara huko Iowa na New Hampshire . Lakini pia inazungumzwa kwenye mikutano binafsi ya wabunge warepublikan huko Capital Hill. Haya ni mabadiliko makubwa kwa chama cha Republikan na inatishia uwezo wao wa kushinda uchaguzi wa kitaifa.”

Mpasuko huo ulikuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu amesema mbunge mrepublikan Vin Weber. Warepublicasn wameahirisha upigaji kura kumchagua spika kwa muda usojulikana na Spika Boehner ataendelea hadi atakae chukua nafasi yake atachaguliwa.

XS
SM
MD
LG