Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 14:21

Bunge la Libya laongeza muda wake wa utawala.


Mwakilishi wa Libya kwenye Umoja wa mataifa, Bernardino Leon, akizungumza na waandishi huku wabunge wa Libya wakisikiliza huko Rabat, Morocco, Sept. 18, 2015.
Mwakilishi wa Libya kwenye Umoja wa mataifa, Bernardino Leon, akizungumza na waandishi huku wabunge wa Libya wakisikiliza huko Rabat, Morocco, Sept. 18, 2015.

Bunge la Libya linalotambuliwa kimataifa siku ya Jumatatu liliongeza muda wake wa utawala kabla ya muda wake wa Oktoba 20, kumalizika, hatua ambayo inaweza kuzusha utata katika juhudi za kuleta amani zinazosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa bunge alieleza kwamba upigaji kura wa Jumapili kuwa ni hatua ya tahadhari ikiwa mazungumzo ya kisiasa yatashindikana ili kuepuka ukosefu wa utawala wa kisiasa nchini humo.

Maafisa wa Umoja wa mataifa wanaojaribu kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa huko Libya waliweka tarehe ya Oktoba 20 kuwa siku ya mwisho ya mazungumzo na kupatikana serikali na hivyo kulivunja bunge hilo. Hivi sasa haijulikani wazi nini kitakachotokea sasa.

XS
SM
MD
LG