Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 15:40

Miili zaidi yapatikana ufukwe wa Libya.


Wakimbizi katika bahari ya Mediteranean.

Msemaji wa hilali nyekundu ya Libya amesema Jumapili kwamba, miili ya wahamiaji wasiopungua 95 imepatikana kwenye ufukwe wa bahari ya Mediterreanean huko Libya mnamo siku 5 zilizopita.

Mohamed Al Masrati amesema maskauti wa hilali nyekundu wamegundua miili 85 kati ya hiyo karibu na mji mkuu wa Libya Tripoli na 10 karibu na Sabartha mji wa pwani wa Libya ambao ni makao makuu ya kuanza safari za boti za walanguzi kuwasafirisha watu kinyume cha sheria na kuwapeleka Ulaya .

Amesema wengi waliofariki dunia ni raia wa nchi mbali mbali za Afrika na juhudi za kutafuta miili zinaendelea. Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM linaeleza kwamba zaidi ya watu 2,600 wamefariki baharini kwa mwaka huu pekee.

XS
SM
MD
LG