Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 01:45

Jukwaa la wahariri lapinga matamshi ya tume ya uchaguzi Tanzania.


Msemaji wa Jukwaa la wahariri Tanzania Bw.Neville Meena.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania (NEC) Jaji Damian Lubuva amezungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini humo alhmisi juu ya utendaji wa vyombo hivyo na majukumu yao kuelekea siku ya kupiga kura.

Akizungumza na Sauti ya Amerika msemaji wa Jukwaa la wahariri Neville Meena amesema "hiki ni kipindi cha mawimbi mazito ya kisiasa na siasa za Tanzania zimebadilika sana".

Vile vile aliongeza kwamba uchaguzi una ushindani wa hali ya juu na kusema tume imewashutumu kwamba vyombo vya habari vinaripoti kauli mbali mbali za viongozi wa kisiasa ambazo wakati mwingine zinaashiria uvunjifu wa amani, kauli za kashfa na vitu kama hivyo.

Mahojiano na Neville Meena
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:03 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Lakini akahoji kwamba tume hiyo imesaini maadili na vyama vya siasa kuhusiana na jinsi ya kuendesha kampeni. Kwa hiyo alishangaa kwanini mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anarundika lawama kwa vyombo vya habari, wakati ameshindwa kudhibiti haki ya kampeni katika nchi.

XS
SM
MD
LG