Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 15:09

Kenyatta atoa wito kusaidia juhudi za kikanda kusitisha mapigano


Rais Uhuru Kenyatta akizungumza kwenye baraza kuu la Umoja wa mataifa jijini New York..
Rais Uhuru Kenyatta akizungumza kwenye baraza kuu la Umoja wa mataifa jijini New York..

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amehutubia mkutano wa 70 wa baraza kuu la Umoja wa mataifa jijini New York Jumatatu akiitaka jumuia ya kimataifa kutoa msaada zaidi kusaidia juhudi za kikanda kusitisha mapigano huko Somalia Sudan Kusini, na mataifa mengine ya Afrika.

Katika hotuba yake alizingatia zaidi juhudi za Kenya katika dhamira ya nchi yake kuendelea kuwa na jukumu muhimu katika kukuza na kuimarisha usalama wa kikanda , na kuimarisha majukumu yake katika kuendeleza ushirikiano wa kimataifa.

Kwa upande wake rais Yoweri Museveni wa Uganda amekosowa vikali ukosefu wa mageuzi katika mfumo wa umoja wa mataifa na kazi hasa za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa. Hata hivyo alitoa wito wa kuwepo na ushirikiano wa dhati kati ya umoja wa mataifa na jumuiya za kikanda na mashirika ya kikanda katika kuleta mageuzi ya kweli kwenye umoja wa mataifa na baraza la usalama.

Wakati huo huo Rais Barack Obama aliongoza kikao maalum cha viongozi juu ya kazi na majukumu ya idara ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa. Katika mkutano huo kiongozi huyo wa Marekani alitangaza kwamba mataifa 50 ya dunia yameeleza dhamira yao kuongeza hadi wanajeshi elfu 30 kwa kikosi cha kulinda amani, pamoja na kutolewa helikopta na vifaa zaidi vinavyohitajika kuhakikisha kazi zake zinafanyika kama inayohitajika kuleta utulivu na uthabiti katika maeneo 16 ya dunia inayofanya kazi.

Mbali na mkutano mkuu kumekuwepo na mikutano mbali mbali ya kando. Umoja wa Afrika ulikua na mkutano wa siku nzima kujadili utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo endelevu SDG yaliyopitishwa mwishoni mwa wiki na mwenyekiti wa kamisheni ya AU Bi. Dlhamini Zuma .

XS
SM
MD
LG