Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:57

Obama amkaribisha Papa Francis White house


Rais wa Marekani Barack Obama, na mke wake Michelle Obama, na Papa Francis wakipungia wati waliojitokeza huko White House Washington, Sept. 23, 2015.
Rais wa Marekani Barack Obama, na mke wake Michelle Obama, na Papa Francis wakipungia wati waliojitokeza huko White House Washington, Sept. 23, 2015.

Rais Barack Obama alimkaribisha Papa Francis White House kwenye mapokezi maalum yaliyofanyika kwenye bustani ya ikulu huku kukiwa na watu 15,000.

Siku ya kwanza ya Papa Francis hapa Marekani ataitumia kuzungumza na Rais Obama, pamoja na kuzungumza na maaskofu wa Marekani na kumtangaza mtakatifu mmishenari wa karne ya 18 Mhispania aliyetangaza neno la mungu katika eneo ambalo sasa ndio Calirfornia.

“Ninaamini hamasa katika ziara yako si tu kwa sababu wewe ni Papa lakini pia ni kwa sababu ya utu wako wa kipekee. Katika unyenyekevu wako, kupenda kuwa mtu wa kawaida, maneno yako mazuri na ukarimu wa roho yako” Obama alisema akimkaribisha Papa.

“Unatukumbusha kwamba katika macho ya Mungu kipimo chetu kama watu mmoja mmoja na jamii hakitokani na utajiri au madaraka au kituo au umaarufu lakini ni kwa jinsi gani tunavyofuata maandiko na wito wa maandiko wa kuwainua masikini na waliotengwa na kutetea haki na kupinga kutokuwa na usawa kwasababu wote tumeumbwa katika sura ya Mungu” alisema.

Katika hotuba yake Rais Obama aliongelea kuhusu wakimbizi ambao wanakimbia maeneo yalioharibiwa na vita, uhuru wa kuabudu na jukumu takatifu la kulinda dunia na kumshukuru Papa kwa juhudi zake za kuboresha mahusiano kati ya Cuba na Marekani.

Papa Francis alielezea historia yake kama mtoto wa mhamiaji katika maneno yake ya ufunguzi hapo White house na kuliweka suala la wakimbiuzi kuwa la umuhimu wa juu katika ziara yake ya Marekani.

XS
SM
MD
LG